BREAKING: Mwigizaji Maarufu Hashim Kambi Afariki Dunia | Bongo Gossip Tz

Muigizaji nguli wa Bongo Movie, Hashim Kambi amefariki dunia ghafla leo baada ya kuanguka akiwa katika majukumu yake ya kazi.


Hashim Kambi anakumbukwa kwa kipaji chake cha kipekee na mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu nchini, ambapo aliweza kugusa maisha ya watu wengi kupitia sanaa yake. Kuondoka kwake ni pigo kubwa kwa wadau wa filamu na taifa kwa ujumla.


Familia, ndugu, jamaa na mashabiki wake wameendelea kuomboleza msiba huo mkubwa. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi. Amina. 🤲



Comments