Ukimpoteza mtu huyu katika maisha yako.. UTAJUTA..

 

Kuna watu ukiwapoteza katika maisha yako, huenda ukajikuta unajilaumu sana baadaye si kwa sababu huwezi kuishi bila wao, bali kwa sababu walikuwa na thamani ya kipekee ambayo huioni mapema. Hawa hapa ni aina tano:


1. Mtu anayekupenda kwa dhati bila masharti

Huyu hakupendi kwa sababu una pesa, mwonekano au nafasi. Anakupenda kwa wewe ulivyo. Anakuvumilia, anakuelewa, na anakutakia mema kweli. Ukimpoteza, kupata mtu wa aina hiyo tena si rahisi.


2. Mtu aliyekuwa anakuinua wakati unaanguka

Huyu ni yule anayekutia moyo unapofeli, anakusukuma usikate tamaa, na anakukumbusha uwezo wako wakati wewe mwenyewe huoni thamani yako. Ukimpoteza, unaweza kukosa mtu wa kukuamsha tena kiakili na kihisia.


3. Mtu aliyekusamehe mara nyingi

Huyu amevumilia makosa yako, hasira zako, na wakati mwingine hata upumbavu wako. Lakini bado alibaki. Ukimpoteza, unaweza kugundua si kila mtu ana moyo wa kusamehe mara nyingi hivyo.


4. Mtu aliyekupigania bila kuchoka

Huyu hakukata tamaa juu yako hata wakati wewe ulijikata tamaa mwenyewe. Alikupigania mbele ya watu, alisimama upande wako hata ulipokosea. Ukimpoteza, utajua thamani ya mtu anayepigania uwepo wako.


5. Mtu aliyekua amani yako

Huyu alikuwa anakufanya utabasamu bila sababu kubwa, anakupa utulivu wa moyo, na uwepo wake ulikuwa kama pumzi ya amani. Ukimpoteza, unaweza kuhisi pengo ambalo si rahisi kulijaza.

Comments

Popular Posts